Monday, March 31, 2014
BUNGE LA KATIBA KUANZA KAZI RASMI LEO.
Do you like this story?
Wakati bunge la katiba leo
linaanza kujadili sura mbili za
rasimu ya katiba ambazo zitalenga muundo wa muungano, umoja wa katiba wa wananchi (ukawa) umewataka wajumbe wake kutokuondoka
Dodoma hadi kumaliza kujadili sura hizo.
Kwa mujibu wa ratiba ya bunge iliyotangazwa ijumaa
iliyopita na makamu wenyekiti wa bunge hilo, samia saluhu leo wajumbe
watanza kujadili sura ya kwanza ya
rasimu ambayo inahusu jina mipaka, alama
lugha na tunu za taifa.
Sura ya sita inahusu
muundo wa muungano vyombo vya
utendaji na mamlaka ya serikali nchi
washirika na uhusiano wan chi washirika.
Katika bunge la katiba yahaya
hamis hamad alisema utaratibu wa kujadili rasimu kwa kuanza na sura hizo
umetolewa na kamati ya uongozi kwa
kuaingatia kanuni 58 ya bunge la katiba.
Kanuni hiyo ya 58 inasema
kamati ya uongozi itakuwa na majujumu ambayo ni (a) kujadili na kuamua mambo
yote yanayohusu uendeshaji bora wa
shughuli za bunge maalumu na kamti zake. B kujadili na kupanga ratiba ya
utekelezaji wa shughuli za bunge na ( c
) kujadili na kufanya uamuzi kuhusu masuala yanayohitaji usuluhishi na
maridhiano.
Mjumbe wa bunge hilo john mnyika akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti
wa ukawa freeman mbowe alisema
kaunzia leo bunge litaanza kujadili
muundo wa muungano ambao alisema
ndiyo moyo ya rasimu ya katiba hivyo wajumbe wote wa ukawa watashiriki.
Tumewaomba wajumbe
kutokuondoka wakati wa kujadili sura hizi mbili kwani ndiyo roho ya rasimu na
tunaonya ikifika hatua CCM wakachakachua tutachukua maamuzi mazito na gharama zozote alisema mnyika.
Mnyika alisema tayari
wamepata taarifa kuwa wajumbe kutoka CCM
wataingia na mapendekezo yao na
yatapigiwa kura kwa kujua wao wapo wengi
pamoja na uteuzi wa wajumbe 201
walioteuliwa na rais jakamya kikwete.
Hata hivyo alisema wakati
wa kupitisha vifungu vya rasimu hiyo ni wazi kuwa CCM hain a theluthi mbili kwa
Zanzibar na kama wakipeleka mapendekezo
ya kutaka kuvunja sheria na
kanuni kwa masilahi yao hawatakubali.
Myika amesema licha ya
mwenyekiti wa kamati ya mabadiliko ya
katiba jaji joseph warioba kueleza
upungufu wa mfumo wa serikali mbili na
hivyo kupendekeza serikali tatu ambyo ni maoi ya wnanchi bado CCM inashinikiza
na kutetea msimamo wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BUNGE LA KATIBA KUANZA KAZI RASMI LEO.”
Post a Comment