Monday, March 31, 2014

LOWASSA: HAKUNA KAMA EDWARD SOKOINE.




Waziri mkuu mstaafu Edward lowassa amesema viatu vya hayati waziri mkuu wa tatu Edward  sokoine ni bikubwa sana kwamba havivaliki.

Lowassa aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma jana.

Mkutano ulisitishwa  na mtoto wa hayati sokoine namelok kwa ajiliya mazungumzo  maadhiisho ya miaka 30 tangu kifo cha baba yake, kilichotokana na ajali ya gari dakawa  mkoani morogoro.

Havivaliki vile viatu ni vikubwa sana tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini marehemu alisema kumtimikia binadamu ni heshima alisema  wkati akijibu swali aliloulizwa  yeyey kama mbunge wa monduli anadhani ni kwa kiwango gani anaweza kuvaa viatu vya sokoine.

Amesema  eneo ambalo aliliamini snaa hayati sokoini ni kujenga shule za wasichana  hasa kwa wafugaji.

Amesema kwa kushirikiana na askofu denis wa kanisa katoliki nchini walitenga eneo monduli juu kwa ajili ya ujenzi wa shule ya wasichana ya nyakazangai ambayo tayari  imeshajengwa.

Aliseme pia  wamejenga shule mbili ambapo moja ilijengwa na kanisa la kiingili  la kilutherani (KKKT) na nyingine imejengwa  kwa utaratibu  wa shule za kata.

Aliamini mifugo lazima  iwe na maeneo mazuri na alitenga maeneo kwa ajili ya wakulima  na wafugaji eneo ambalo wameheshimu sana utaratibu  huu ( wa kutenga maeneo)  ni monduli pale mambo yanakwenda  vizuri alisema.

Alimshukuru raisi kikwte aliyewasaidia sana wafugaji kwa kuwapatia sh 3 milioni kwa ajili  ya ukarabati wa mabawa yaliyopasuka kutokana na mvua kubwa mwaka juzi ahuku akiongeza kuwa  walipata  shida ya njaa kubwa na kupotea kwa mifugo mingi lakinirais kikwete aliwapatia mifugo 604 ambayo nayo iliwasaidia sana.

0 Responses to “LOWASSA: HAKUNA KAMA EDWARD SOKOINE.”

Post a Comment

More to Read