Monday, March 31, 2014

MWANGUNGA : PILIPILI USIYOILA YAKUWASHIA NINI?




Waziri wa zamani  wa maliasili na utalii shamsa mwangunga amewapiga kijenge wabunge  wengine  akisema pilipili uliyokula inakuwashia nini?

Mwangunga alizungumzia sakata la kupiga  kura ya siri  au ya wazi alisema labda niseme kwa kifupi sana kwa sabab u sina mengi  ya kuzungumza  nimalizie kwa kusema kuwa pilipili uliyoila yakuwashia nini?

Mjumbe huyo alisema kuwa wanaotaka kura za siri ni wanafiki kwani wanaficha nini kwa watu ambao waliwatuma kuingia bungeni humo.

Amesema kuwa kipenda roho ni kwa mtu kula nyama mbichi hivyo pendekezo la wajumbe kupiga kura za wazi  au ya siri ni pendekezo zuri  ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mtu.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo suala la kulazimisha baadhi ya watu  kuingia katika mfumo wa kupiga kura ya siri ni dalili za woga usio na mantiki  katika karne ya sasa.

Naye masoud abdalah salim alizungumzia  uamuzi wa kupiga kura mseto akisema  itakuwa ni kioja kupiga  kura za aina mbili katika uamuzi wa jambo moja.

Salim alipendekeza kuwa  kura ya siri ndiyo inayowafikisha watu mahali ambapo ni salama.

0 Responses to “MWANGUNGA : PILIPILI USIYOILA YAKUWASHIA NINI?”

Post a Comment

More to Read