Monday, March 31, 2014

TMA YAONYA UWAPO WA KIMBUNGA, MVUA.




 mamlaka ya hali ya hewa TMAA imetahadharisha  juu  ya kuwapo kwa kimbunga  kitwacho  chellen katika mwambao  wa bahari ya hindi ambacho kitasababisha mvua  kubwa inayozidi mililita 50  ndani ya masaa 24  kuanzia jana katika mikoa 24.

Taarif aya mamalaka hiyo ambayo imetolewa jana kwa vyombo vya habari imebainisha kuwa mvua  zitanyesha katika mikoa ya dare s salaam, mtwara, lindi, tanga,unguja, pemba, singida, Dodoma, Ruvuma, katavi, njombe, mbeya na morogoro.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mvua hiyo itarajia kuanza jana zitaendelea hadi april mosi mwaka huu na wakazi wa mkoa hiyo  watuamiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa zimetakiwa kuchukua tahadhali  zinazotakiwa.

Imebainisha kuwa uwezo wa mvua hiyo ni asilimia 80 na mwendelezo  wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha  nchi nzima katika baadhi ya maeneo ambako hupata  misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Mamlaka ya hali ya hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana alisema sehemu ya taarifa  hiyo na kuongeza kuwa uangalifu na tahadhari vinahitajika ili kuepusha maafa zaidi.

0 Responses to “TMA YAONYA UWAPO WA KIMBUNGA, MVUA.”

Post a Comment

More to Read