Thursday, March 6, 2014

KAMPENI HOMA YA INI KUZINDULIWA KESHO.




KAMPENI ya ugonjwa wa Homa ya Ini unaosambazwa na Virusi vya Hepatitis B itazinduliwa rasmi kesho Ijumaa, Machi 7, mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Ilala–Amana, jijini Dar es SalaAkizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inayoendesha kampeni hiyo, Eric Shigongo amesema, kama kampuni wameguswa na ugonjwa huo hivyo wamedhamiria kupambana kwa nguvu zote kuzuia ugonjwa huo.
“Homa ya Ini ni ugonjwa hatari sana, maana ukimpata mtu kinachofauata ni kifo. Naweza kusema ni ugonjwa hatari zaidi kuliko hata Ukimwi, lakini tofauti yake na Ukimwi ni moja; huu una kinga.

“Ni lazima tuungane kama taifa, huu ugonjwa ni hatari sana, sisi Global Publishers tumeanza, kinachofaa ni wewe na yule kujitokeza ili tuishinde hii vita pamoja. Kesho tutazindua rasmi,” alisema Shigongo na kuongeza:

“Ndugu zetu wengi sana wanapoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huu wa Homa ya Ini, lakini kwa sababu chanjo ipo, lazima tuchukue hatua. Sisi Global Publishers tumeamua  kuchukua jukumu la kuhakikisha Hepatitis B unatokomezwa.

“Naomba watu wajitokeze wengi ili tuizindue kwa kishindo kampeni hii. Lazima tuhakikishe tunapigania  maisha ya Watanzania ili wasipate ugonjwa huu hatari ambao hauna tiba lakini uzuri ni kwamba una kinga.”

Aidha, Shigongo alisema kampeni hiyo itaendeshwa kwa miezi minne mfululizo kabla ya kufikia kilele chake Julai 28, mwaka huu.

Kampeni hii inaendeshwa na Global Publishers kwa kushirikiana na Hospitali ya Amana, Megra Clinic, Sanofi Pasteur, Damu Salama na SD Africa.

0 Responses to “KAMPENI HOMA YA INI KUZINDULIWA KESHO.”

Post a Comment

More to Read