Thursday, March 6, 2014

MBUNGE ATOA MPYA BUNGENI




Tangu kuanza kwa bunge Maalumu la Katiba mwezi februari 18 mwaka huu kumekuwa a vituko vingi, lakini kali zaidi ilikuwa wakati Mbunge wa Chambani (CUF) Yussuf Salim Hussein alipotishia kuwazoea wajumbe wenzake juzi.

Mjumbe huyo alitoa tishio hilo baada ya kuzuiwa kuchangia mjadala kuhusu rasimu ya kanuni za Bunge hilo na badala yake mjumbe mwenzake, Peter Serukamba (CCM) alipewa nafasi na mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo . Pandu Ameir Kificho.

“ Ninyi hamnijui mimi. Nasema hivi nitawazomea wote humu ndani . nyinyi vipi bwana nitawazomea mimi nasema nitawazomea ngojeni tu” alisema mjumbe huyo kwa lahaja ya kiunguja huku wajumbe kuangua kicheko.

Hata alipokaa, aliwageukia wajumbe wenzake waliokuwa wamekaa viti vya nyuma na kusisitiza kauli yake kutaka uwazomea.

Baada ya kukaa, Hussein hakupea nafasi nyingine ya kuzungumza licha ya kuonekana mara kadhaa akisimama na kunyoosha kidole, kuashiria kuwa alikuwa na jamboa la kuchangia.

Akizungumza nje ya Bunge hilo, Hussein amesema: “Nilikuwa nataka kuzungumza jambo la maana kweli ila ipo siku nitapata nafasi ya kulizungumza

0 Responses to “MBUNGE ATOA MPYA BUNGENI”

Post a Comment

More to Read