Sunday, March 23, 2014
MABOMU YARINDIMA KWENYE MACHIMBO NZEGA, MBUNGE DKT KIGWANGALA AKAMATWA NA POLISI.
Do you like this story?
Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora. |
Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora
limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya
dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa
machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited
wilayani Nzega.
Mara
baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa
yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla polisi waliibuka na
kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt
Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo alifanya mkutano
wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao
ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini nchini Paul Masanja
kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.
Kufuatia
malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali gharama waliozotumia
walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo la machimbo ndipo
mkutano ukavunjika na maandamano yakaanza na matokeo yake mabomu ya machozi
pamoja na risasi za moto.
Katika na purukushani hizo polisi walifanikiwa
kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la
uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Katika
hatua nyingine hali ilikuwa tete kwa waandishi wa habari kwani askari wa jeshi
hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho
mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya
wachimbaji kujitokeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MABOMU YARINDIMA KWENYE MACHIMBO NZEGA, MBUNGE DKT KIGWANGALA AKAMATWA NA POLISI.”
Post a Comment