Sunday, March 23, 2014
WALIOBA: TUMEMALIZA KAZI YETU”.
Do you like this story?
Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete
kuzindua Bunge na kuponda ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwenyekiti wa
Tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema jukumu walilopewa kwa mujibu wa sheria
wamelikamilisha na wanawaachia wananchi waamue.
Akizungumza na Mwananchi jana asubuhi, Jaji
Warioba alisema alichokizungumza Rais Kikwete ni maoni yake na kwamba hawezi
kuyajadili.
“Rais Kikwete alichozungumza ni maoni yake,
kwa sasa sipendi kuyazungumzia hayo, ” Jaji Warioba alieleza.
Alisema wamemaliza jukumu walilopewa na
kwamba sasa jukumu lote lipo mikononi mwa Bunge.
Jaji Warioba alisema Tume yake ilikusanya
maoni kutoka kwa wananchi, mabaraza ya wilaya ya Katiba na Taasisi mbalimbali,
wakatengeneza rasimu ambayo sasa wameikabidhi kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Jaji Warioba pia alikataa kuzungumzia zogo
lililoibuka bungeni na kusababisha rasimu kuwasilishwa Jumatano, baada ya kikao
cha Jumanne kuvunjika.
Hali hiyo ilitokana na UKAWA kudai muda wa
saa 1:30 uliokuwa umepangwa Jaji Warioba ahutubie bungeni uongezwe na kanuni
inayoelekeza Rais Jakaya Kikwete ahutubie kabla Jaji Warioba hajawasilisha
rasimu izingatiwe, baada ya kutangazwa kuwa Rais angehutubia baada ya rasimu
kuwasilishwa.Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu
alisema alitarajia Rais Kikwete angezindua Bunge Maalumu na siyo kutoa maagizo
na vitisho kwa wajumbe.
Alisema hajui lengo la Rais kufanya
alichofanya lakini ana hakika kwa kutoa ufafanuzi wa hoja zilizotokana na maoni
ya wananchi ndani ya rasimu, ameingilia kazi za Tume na hivyo amevunja Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83 toleo la mwaka 2012), inayosema:
“21.-(b) atakayejifanya kuwa mjumbe wa Tume
au Sekretarieti; au (c) atakayeendesha programu ya elimu juu ya mabadiliko ya
katiba kinyume na masharti ya sheria hii, atakuwa ametenda kosa.
(3) atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
kinyume na Sheria hii, atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh2,000,000
(milioni mbili) na isiyozidi Sh5,000,000 (milioni tano) au kifungo kwa muda
usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka mitatu au adhabu zote mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOBA: TUMEMALIZA KAZI YETU”.”
Post a Comment