Monday, March 24, 2014

MBUNGE WA CCM AWEKWA MAHABUSU.




Jeshi la polisi wilayani nzega mkoani hapo limemkamata  mbunge  wa jimbo la nzega (CCM) DK hamis kigwangala  kwa kudaiwa kuhamisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu  kupinga kufungwa kwa machimbo ya mwashina yaliyo jirani  na mgodi wa resolute Tanzania limited.

Kabla ya hapo mbunge huyo alidaiwa  kufanya mkutano mkubwa wa hadhara  na wachimbaji hao katika kijiji cha nzega  ndogo wilayani hapa  na alielezwa matatizo ya kufungwa  kwa machimbo hayo  na kamishana wa madini nchini Paulo Masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao kwenye eneo  hilo.

Katika mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vyema serikali iangalie haki zao katika uendeshaji na uchimbaji wa mashimo hayo kuliko kuwafungia bila kujali ingawa eneo  hilo liko  ndani ya leseni ya mgodi wa resolute lakini wao ndiyo wamiliki wa ardhi hiyo.

Wachimbaji hao walimwomba mbunge  huyo kuambatana nao kwenye maandamano  ya amani kutoka kijiji cha nzega  ndogo kwenda mwashina yalipo machimbo yaliyofukiwa, umbali wa zaidi ya kilomita tatu ili kujionea halihalisi ya kufukiwa kwa eneo hilo na ikiwezekana kufanya  mkutano  mwingine wa hadhara kijijini hapo.

Kufuatilia  hali hiyo wachimbaji hao walianza  maandamano  ambayo yaliungwa mkono  na mbunge huyo hadi kijiji cha mkwajuni  kabla ya kufika  mwashina polisi waliiba  na kuyasambaratisha  maandamano  hayo kwa mabomu ya machozi na risasi  za moto.

Katika  na purukushani  hizo polisi walimkamata  mbunge huyo na kumjeruhi  mtu mmoja kwa risasi kwenye paji la uso na kuondoka naye pamoja na mbunge huyo.

Kamanda wa polisi mkoani tabora susan kaganda amesema hana taarifa yoyote.


0 Responses to “MBUNGE WA CCM AWEKWA MAHABUSU.”

Post a Comment

More to Read