Monday, March 24, 2014

SULUHU AMEKEA UTORO.




Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba, samia suluhu amewataka wajumbe wa bunge hilo kujitahidi  kuhudhuria  vikao vya chombo  hicho  kuwa ndiyo kazi iliyowaleta mjini hapa.

Suluhu amesema hayo muda mfupo kabla ya kuahirisha  semina ya kanuni za uendeshaji kwa wabunge hao.

“Tumekuja  kwa kazi hii ( ya mchakato  wa katiba) kwa hiyo waheshimiwa  wajumbe wajitahidi kuwepo ndani ya bunge  kwa wakati alisema.

Mwananchi alishuhudia  viti vingi vya bunge hilo  lenye wabunge 629  vikiwa tupu baada ya wabunge  wengi kutoingia ndani  ya ukumbu huo jioni ama kuinga na kutoka kabla  bunge hilo halijaairishwa.

Kwa mujibu wa katiba iliyotangazwa asubuhi juzi na mwenyekiti  wa bunge hilo Samuel sitta semina hiyo ilitakiwa  kumalizika saa 2: oo usiku.

Tatizo kama hilo la utoro limekuwa likikemewa mara nyingi na spika wa bunge la jamuhuri ya muungano  anne makinda.

Mara kadhaa tatizo  hilo limekuwa likisababisha kukwama kwa maamuzi muhimu  yanayohitaji  kuamuliwa na wabunge hao.

0 Responses to “SULUHU AMEKEA UTORO.”

Post a Comment

More to Read