Monday, March 24, 2014

USHAMBA ULITUFANYA TUSHINDWE KUCHANGIA.




Mjumbe wa bung la katiba elias  masamaki  amesema wajumbe 201 walioteuliwa na rais  walipata ugumu kuchangia mjadala  bungeni kwa sababu  hawakujua lugha za kibunge  ikiwamo miongozo  na taarifa.

Masamaki ambaye anatokea  kundi la watu wenye ulemavu aliomba akisema: “mara taarifa na wakati mwingine mwongozo  sisi wengine hatujazoea  kutumia maneno hayo  jambo ambalo linatufanya  wakati mwingine kushindwa  kuelewa  tuingizie wapi maneno  haya alisema masamaki.

Hata hivyo amesema kadri wanavyoendelea  kuhudhuria  vikao vya bunge hilo  ndivyo wanavyozidi kuelewa jinsi ya kutuma maeneno  hayo katika kuomba  nafasi za kuchangia.

Wajumbe wanaounda bunge hilo lilianza kazi ya kupitia rasimu  ya pili ya katiba February 18 mwaka huu ni pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi  Zanzibar  wabunge hao  wa bunge wa bunge la jamhuri  wa Tanzania  na kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na rais kutoka  makundi mbalimbali

0 Responses to “USHAMBA ULITUFANYA TUSHINDWE KUCHANGIA.”

Post a Comment

More to Read