Monday, March 24, 2014
IKULU: KUJADILI HOTUBA YA JK KUPOTEZA MUDA.
Do you like this story?
Mkurugenzi wa
mawasiliano ya Rais I kulu salva
rweyemamu amesema kuendela
kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa kwenye bunge hilo la katiba
mwisho mwa wiki ni kupoteza muda.
Akizungumza jana rweyemamu
aliushangaa umoja wa katiba ya wananchi (ukawa)
kuendela kutoa matamko yanayopinga
hotuba hiyo, akisema haumtendea
haki mkuu huyo wan chi na watanzania wote kwa ujumla amesema kama mtanzania
Rais alitoa maoni yake na amekuwa
muungwana kwa kuwambia kwamba bado
wana fursa ya kujadili na kuleta
mapendekezo yao lakini wajali
zaidi maslahi ya taifa.
Hiyo ni propaganda
isiyokuwa na maanda kwa taifa na hata
hatima ya katiba yenyewe. Ningependa kuwakumbusha kwamba watanzania
wamewapeleka Dodoma wakajadili katiba siyo kufanya propaganda tunawataka
wakafanye kazi alisema rweyemamu.
Kwa mujibu wa
rweyemamu umoja huo wenye viongozi kutoka vyama vya upinzani
haumtendei haki Rais kwani kama
mtanzania mkuu huyo wan chi ana fursa ya
kutoa maoni yake.
“wasifikiri kwa kujibu
hivyo Rais wanajibizana na CCM. Rais ni mkuu wan chi ana maoni yake lakini zaidi
ya yote, bunge la katiba siyo mahali pa
kufanya siasa kama wanataka siasa tunawaomba warudi maofisini mwao wakafanye siasa, pale
tumewatuma kazi alisisitiza.
Rweyemamu alibainisha kuwa
mchakato wa kutunga katiba unahitaji
busara na hiyo haiwezi kupatikana kama watu wanatumwa kuwawakilisha wananchi wameamua kufanya siasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “IKULU: KUJADILI HOTUBA YA JK KUPOTEZA MUDA.”
Post a Comment