Saturday, March 8, 2014
MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI MBEYA DR MARRY MWANJELWA ATOA SOMO KWA AKINA MAMA WENZAKE.
Do you like this story?
Afisa Maendeleo ya jamii jiji Mwenye
Suti nyeusi Ndugu Vicent Msolwa akiwa pamoja na mgeni rasmi katika maadhimisho
hayo Daktari Marry Mwanjelwa wakiwa makini kufuatilia yanayo endelea katika
maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mbeya (CCM) Daktari Marry Mwanjelwa akiangalia moja ya kazi za kikundi cha (Eden Women Group)kata ya uyole kati jijini Mbeya |
Akina Baba nao hawakuwa Nyuma katika
kuwa sindikiza akina mama kusherekea siku yao
|
Wanawake Wanaweza |
Wito
umetolewa kwa wanawake jijini mbeya kuhakikisha wanaacha tabia ya kulalamika
na kukata tamaa badala yake wajikite katika kufanya kazi kwa bidii na kutumia
fursa walizo nazo.
Kauli
hiyo imetoleaa leo jijini Mbeya na Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mbeya Dr Marry
Mwanjelwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani
ambapo kila mwaka husherekewa machi8 ambapo pia kilele cha maadhimisho hayo kwa
jiji la mbeya zimefanyika katika viwanja vya ccm Ilomba.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo mbunge huyo amedai kuwa umefika wakati wanawake
wakaacha tabia ya kulalamika badala yake watumie fursa walizo nazo
katika kujiingizia kipato.
Amesema
umefika wakti sasa wanawake wote wakajitambua na kuacha tabia hiyo kwani
imechangia kwa kiwango kikubwa kuendelea kuleta manyanyaso kwa mwanamke huyo.
Hata
hivyo Mbunge huyo amesisitiza suala la kujiamini kwa akina mama ili kuleta
chachu ya mabadiliko dani ya familia na jamii kwa ujumla badala ya kuendelea
kutegemea mwanaume kwa kila jambo katika suala la maamuzi.
Pamoja
na kuwataka akina mama hao kutambua fursa na kujiamini pia amessistiza suala la
kupendana wao kwao ili kuleta nguvu ya pamoja katika kupigania haki zao.
Kwa
upande wao baadhi ya akina mama waliohudhuria sherehe hizo wametoa wito kwa
mashirika mbalimbali ya kijamii kuendelea kutoa elimu kwa akina mama wengine
walipo maeneo ya vijini ili kusaidia kuleta mabadailiko zaidi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI MBEYA DR MARRY MWANJELWA ATOA SOMO KWA AKINA MAMA WENZAKE.”
Post a Comment