Wednesday, March 5, 2014

N'GOMBE 30 WAIBIWA WAKIWA MALISHONI


kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi


JUMLA ya ng’ombe 30 wakiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 15 wameibiwa wakiwa malishoni Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 17:00 jioni katika Kijiji cha  Stamico Kata ya Mkoala wilayani Chunya.

Amesema, mifugo hiyo inayomilikiwa na mfugaji Mihambo Paul(34) mkazi wa Stamico ilichukuliwa na watu wasiojulikana wakati  ikiwa malishoni bila ya msimamizi.

Kamanada Msangi, alisema askari polisi wanaendelea na msako wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Aidha, Msangi aliiomba jamii ya wafugaji kujenga utamaduni wa kulinda au kusimamia mifugo yao kwani maisha ya sasa yameharibika si kama miaka ya nyuma ambayo mtu uweza kuacha kitu chako nje na kisichukuliwe na mtu.

Hata hivyo, aliwaomba wananchi kutoa taarifa polisi endapo wataiona mifugo hiyo sambamba na wahusika wa wizi huo.

0 Responses to “N'GOMBE 30 WAIBIWA WAKIWA MALISHONI”

Post a Comment

More to Read