Wednesday, March 5, 2014

PAPA FRANCIS ASEMA KIPINDI CHA KWARESMA NI WAKATI WA SALA,KUFUNGA NA KUTUBU


Papa francis


Papa ameutaja wakati huu kuwa ni wakati muhimu, ni wakati wa kupiga hatua ya nguvu ya mageuzi kiroho, akimtaka kila Mkristu, kufanya mageuzi ya kutoka nje ya tabia na mazoea mabaya, ovu na udanganyifu.

Aliongeza katika kipindi cha Kwaresima , Kanisa linatoa mialiko mawili muhimu: kwanza kuwa na ufahamu zaidi juu ya kazi ya ukombozi ya Kristo , kuishi na dhamira zaidi kwa mujibu wa ubatizo wetu.

Ufahamu katika maajabu ya Bwana aliyoyafanya kwa ajili ya wokovu wetu, ambayo yanagusa akili na mioyo yetu, katika kujenga tabia ya kutoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya neema zake anazotupatia, kwa kuwa yeye alitimiza yote, kwa ajili ya watu wake na ubinadamu wote.

 Na hili linakuwa ni sababu ya sisi kufanya mageuzi chanya kiroho, kama jibu la kushukuru maajabu ya fumbo la upendo wake wa kukomboa.

Papa ametaja wito wa pili wa Kanisa katika kipindi hiki, ni kufanya mabadiliko na kutembea katika ukweli wa njia Ubatizo, katika maana kujinasua na mazoea mabaya yenye kudhoofisha mwendo katika safari ya kukutana na kutembea pamoja kama jumuiya, Parokia na kama taifa.

 Papa ameasa na kuomba uangalifu dhidi ya pinzani na mashinikizo ya tamaduni, yanayoweza kuwa kikwazo au kuwa kinyume na kumcha Mungu. 

Mashinikizo ya kidunia yanayofanya hata wazazi kupata ugumu wa kufundisha watoto wao faida za kumcha Mungu, kushindwa kufundisha hata ishara ya msalaba.

Maisha ambayo uhalifu wa vita,madhulumu, umaskini na matendo mengine maovu dhidi ya jamii yamegeuzwa kuwa jambo la kawaida.
 Papa alieleza na kukumbuka vurugu na ghasia za mapigano , zinazosikika kila siku katika vyombo vya habari, ambazo zinasababisha mateso kwa watu wake kwa waume. Watu wanao lala mitaani, ambao hawana tena makazi . 

Watu walio lazimika kuwa wakimbizi, wale wanao tafuta uhuru na heshima yao, inayokataliwa kama vile si haki msingi.

Papa aliendelea kusema, tumekuwa na mazoea ya kuishi katika jamii isiyojali uwepo wa Mungu, yenye kujidai inaweza kuishi bila Mungu na tabia zingine mbovu zisizo kuwa za Kikristo, ambazo hulewesha moyo na matamanio ya starehe za kidunia.

Hivyo kwa Mkristo, kuwadia kwa kipindi hiki cha Kwaresima, unakuwa ni wakati wa unaoongoza katika kufanya mageuzi ya kweli ,ni wakati wa kufanya mabadiliko katika kukabiliana na hali halisi za uovu, kama changamoto katika maisha ya kumfuata Kristu.

 Ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kuonekana, kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla, kupitia njia ya kuiamini Injili na Mungu. 

Kwa njia hii pia inaruhusu sisi kuangalia kwa macho mapya, mahitaji ya ndugu zetu wahitaji. Kwaresima ni wakati mwafaka kwa kubadilika na kumpenda jirani yako , upendo wenye kufahamu majitoleo na ukarimu wa moyo na kwa huruma wa Bwana, anayetuimarisha sisi kwa umaskini wake" (cf. 2 Kor 8.9 ). 

Ni wakati wa kutafakari juu ya fumbo hili, kati imani , upendo , msalaba na ufufuo wa Kristo , tukiwa na utambuzi kwamba, wokovu huu ni zawadi isiyo na kipimo, inayotolewa bure kwetu na mpango wa Mungu.

Papa alikamilisha kwa kutaja mambo muhimu mengine ya kukumbuka katika kipindi hiki cha Kwaresima kwamba, ni pamoja na kumtolea Mungu shukurani kwa ajili ya fumbo hili la upendo wake kusulubiwa, imani ya kweli , yenye kufanya mageuzi na kuufungua moyo wa kuwaona ndugu wengine wahitaji. 

Kwa njia hii, Papa aliomba msaada wa Mama Bikira Maria, Muumini wa kwanza katika Kristo, aungane nasi, wakati huu wa siku za maombi ya nguvu na toba , ili tupate kujitakasa na kufanya upya wa kiroho, katika kuliamini Fumbo kuu la Pasaka ya Mwanae.
chanzo-Vatican radio

0 Responses to “PAPA FRANCIS ASEMA KIPINDI CHA KWARESMA NI WAKATI WA SALA,KUFUNGA NA KUTUBU”

Post a Comment

More to Read