Thursday, March 6, 2014

KANDORO :HAKUNA HAJA YA WAKULIMA KUENDELEA KUWA MASIKINI.


Kandoro akizungumza na wananchi wa vijiji vya jirani na mradi huo wa skimu ya umwagiliaji namna ya kutumia fursa hiyo kujinufaisha badala ya kuacha kilimo na kukimbilia mjini ambako hakuna ajira.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akitoa maagizo kwa uongozi wa kijiji cha Kingili pamoja na viongozi wengine wa Wilaya juu uhamasishaji wakulima kutumia njia bora za kilimo cha mpunga .




Mkuu wa mkoa Mbeya bwana Abasi Kandoro ameuagiza uongozi wa kijiji cha Kingili Kata ya Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kuhakikisha wanahamasisha wakulima juu ya  kuachana  na kilimo cha kizamani  Cha mpunga na kujikita katika ulimaji wa kisasa kwa kutumia njia bora za kitaalam.

Amesema kwa muda mrefu sasa wakulima wamekuwa wakijishughulisha  na shughuli za Kilimo bila kuwa na mafanikio yoyote hasa kutokana na kuendeleza  kilimo cha mazoea.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo Wilayani Kyela Mara baada ya kutembelea mradi wa Kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Kingili kata ya Ipinda mradi ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni28 zilizotolewa na serikali kwa lengo la kuinua kilimo cha umwagiliaji wilayani humo.

Kandoro amesema nivema sasa wakulima wakaachana na kilimo cha mazoea bila kufuata taratibu za kitaamu Hali ambayo ime fanya wakulima wengi kuendelea kuwa masikini na kushindwa kufikia malengo Yao.

Amesema Kilimo cha kutupa kwa mkono ni Kilimo cha kizamani sana ambacho hakiwezi kuwaondoa wakulima hao katika umasikini hivyo umefika wakati kwa viongozi pamoja na wataalamu kushirikiana kwa ukaribu kwa lengo la kumkomboa mkulima huyo.

Amesema katika kuhakikisha mkulima ananufaika na Kilimo chake serikali imeamua kuanzisha mradi wa kukoboa mpunga katika kijiji cha kapusyi wilayani Kyela Mkoani humo ambao umegharimu kiasi cha shilingi milion 200 ambapo  lengo lake ni kumfanya mkulima aendelee kunufaika na zao hilo la mpunga.

0 Responses to “KANDORO :HAKUNA HAJA YA WAKULIMA KUENDELEA KUWA MASIKINI.”

Post a Comment

More to Read