Thursday, March 6, 2014
SUALA LA JINSIA LAIBUA MJADALA MZITO KWENYE BUNGE MAALUM LA KATIBA
Do you like this story?
Bungeni Dodoma |
Suala
la Jinsia katika uongozi wa Bunge Maalum la Katiba limeibua Mjadala mzito
katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Mjumbe
wa Bunge hilo Lediana Mung’ong’o ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua suala hilo
wakati wa mjadala kuhusu marekebisho ya kanuni za bunge kipengele 8(i)
kinachozungumzia utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
Mung’ong’o
alitaka kipengele hicho kuzingatia uhusiano wa kijinsia, ambapo kama mwenyekiti
atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa
mwanamke, makamu wake awe mwanaume.
“Mwenyekiti
hili suala la Mwenyekiti na Makamu wake hatuna budi kuangalia suala la jinsia
kwamba ikiwa mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama
Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume” alisema Mung’ong’o.
Naye
Mjumbe wa Bunge hilo Anna Abdalah alisema kuwa suala hilo lilikosewa Tangu
awali hivyo hakuna budi makubaliano yafanyike kwa busara maana wanawake wenye
sifa na uwezo wapo wengi Tanzania Bara na Zanzibar.
Akichangia
katika suala hilo Mjumbe wa Bunge Hilo ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha
Adam Malima alisema kuwa ili kuwepo kwa amani na Mshikamano sheria haina budi
kusema wazi endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamu wake atoke
Zanzibar.
Akijibu
hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman amesema kuwa suala
hilo liwe la marekebisho lakini si kwa kuvunja sheria hiyo.
“Sharti
hilo likibadilishwa litakuwa ni kituko na tutakuwa tunarekebisha sheria ambazo
hazikutungwa na Bunge Maalum la Katiba hivyo ni busara kufanya makubaliano ili
kufikia muafaka wa jambo hilo" amesema
Othman Masoud Othman.
Othman Masoud Othman.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SUALA LA JINSIA LAIBUA MJADALA MZITO KWENYE BUNGE MAALUM LA KATIBA”
Post a Comment