Sunday, March 16, 2014

RAIS KIKWETE AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA AFRIKA KUSINI MHE MAITE NKOANA-MISHAMBANE LEO IKULU DAR ES SALAAM


:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo



UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
              press@ikulu.go.tz             
Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT’ SOFFICE,
    THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR
ES SALAAM
.
Tanzania.

TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete. 

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
16 Machi,2013

0 Responses to “ RAIS KIKWETE AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA AFRIKA KUSINI MHE MAITE NKOANA-MISHAMBANE LEO IKULU DAR ES SALAAM”

Post a Comment

More to Read