Wednesday, March 5, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.


Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.

Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.

Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.

0 Responses to “RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO ”

Post a Comment

More to Read