Tuesday, March 4, 2014

WACHIMBAJI WADOGO WANUSURIKA KIFO GEITA




GEITA. Watu wawili wameokolewa baada ya kufukiwa na kifusi ndani ya shimo la mita 600 katika kijiji cha chilulumo, Mkoani Geita wakati walipoingia kwa shughuli za uchimbaji mdogo.

Tukio hilo lilitokea wiki ilopita kwa watu hao ambao ni wachimbaji wadogo waliingia ndani ya shimo hilo kwa lengo  la kuchimba dhahabu, lakini wakati wakiwa ndani ya shimo, walisikia kitu chenye mshindo mzito ndipo wakaamua kukimbia ndani zaidi ili kujiokoa.

Wakizungumza baada ya kuokolewa jana baada  ya kukaa ndani ya shimo hilo ndani ya siku nne, wachimbaji hao, Sadick Charles ( 29) na Amuru Seleman (27) walisema waliingia katika shimo hilo saa 2 hasubuhi siku ya alhamis, lakini wakati wakiwa katika shimo hilo walisikia kishindo kwa kuanguka kwa udongo.

 Amesema baada ya kuonga juhudi hizo hazikuzaa matunda wakaamua kutumia zana walizokua nazo kuanza kuchimba eneo ambalo limezibwa ili kujiokoa, lakini pia hazikufanikisha kwani nguvu zilianza kuwaishia na kuamua kuanza kuchimba mashimo ili kupata nafasi kwaajili ya kupata hewa .

Kamanda wa polisi mkoani Geita ,Leonard Paulo alisema baada ya kupata taarifa, walifanya juhudi na serikali ya mkoa, polisi na kampuni ya GGM kufanya uokozi na kufanikiwa kuokoa watu hao. 

0 Responses to “WACHIMBAJI WADOGO WANUSURIKA KIFO GEITA”

Post a Comment

More to Read