Tuesday, March 4, 2014
MTOTO AUNGUZWA KWA KUDOKOA NJEGERE
Do you like this story?
MWANAFUNZI Wa darasa la kwanza shule ya msingi jangwani, manispaa ya
sumbawanga amechomwa moto mikono
yake miwili, kutokana na tuhuma za
kudokoa njegere zilizokua zikichemka
jikoni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Jacob Mwaluanda amethibitisha mkasa huo aliouita ni wa kikatili huku
akimtaja mtuhumiwa kua ni
Anifa Lunyerere (18) mkazi wa kitongoji
cha bangwe manispaa ya sumbawanga .
Kamanda Mwaruanda
amesema Lunyerere alimchoma mtoto huyo (jina limeifadhiwa ) wiki iliyo pita katika kitongoji hicho cha
Bangwe saa sita mchana . kwa mujibu wa
kamanda Mwaruanda, mtoto huyo alipohojiwa alidai alifikia
uamuzi huo wakudokoa njegere baada ya kuzidiwa na njaa , alikua ametoka shuleni ambapo alikua ajala chochote .
‘’ mtoto huyu
alieleza kuwa wifi yake huyo amekua na
tabia ya kumfanyia vitendo vya
kikatili mara kwa mara kama vile kumng’ata mgongon
hata kama hajakosea kitu chochote,’’ alidai kamanda Mwaruanda
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na
anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote
baada ya uchunguzi wa awali
wa shauri lake kamili .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTOTO AUNGUZWA KWA KUDOKOA NJEGERE ”
Post a Comment