Tuesday, March 4, 2014

MJUMBE APONDA WAZEE BUNGENI, AZOMEWA


BUNGENI DODOMA


Mjumbe wa bunge la katiba Shaka Omari Masoud, amesema hatasikiliza maneno ya ushawishi kutoka kwa wazee ambao alidai kibailojia, watakufa lakini yeye baada ya miaka 50 ijayo, atakuwepo kutetea katiba. 

Mjumbe alikuwa akichangia mawazo yake katika mjadala wa kanuni za uendeshaji wa Bunge hilo wiki iliyopita Mjini Dodoma.

“Kwa umri wangu sitasikiliza maneno ya wazee. Kibaiolojia hawa wazee keshokutwa watakufa na mimi nitakuja kusimama baada ya mika 50 kuitetea katiba hii”; alisema hali iliyosababisha baadhi ya Wajumbe kuzomea.

Alisema atakuwa tayari kuzungumza ukweli na kile anachokiamini kuhusu mchakato huo wa kutunga katiba mpya na kwamba hiyo itasaidia kupatikana kwa katiba bora.

“Mtu mzima hatishiwi nyau anasimamia msimamo wake, mimi nashauri tupige kura ya wazi ili kila mtu aandike historia na sisi vijana mnaotuachia nchi tuwe na cha kusimulia”;amesema

0 Responses to “MJUMBE APONDA WAZEE BUNGENI, AZOMEWA”

Post a Comment

More to Read