Tuesday, March 4, 2014

ASKARI FFU ZANZIBAR AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Kamishina wa Polisi Zanzibar (Hamdan Omar Makame)


Askari wa kikosi ch FFU, Mohamed Mjomba (Namba E 5607) ameuawa kwa kupigwa risasi , huku mwingine akijeruhiwa baada ya majambazi kuvamia hotel ya kitalii ya Ponge Bay iliyopo Pongwe Mkoani kusini Unguja.
Amesema jana , Kamishan wa polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame alisema tukio hilo lililotokea juzi saa  3:00 usiku wakati wageni wakiwa wamepumzika na askari hao wa FFU kutoka kituo cha polisi machui wakiwa katika lindo kwenye hotel hiyo.

Kamishan Hamdani amesema muda huo lilifika gari moja na baada ya kuegeshwa watu watatu waliteremka na kumvamia askari mwenye namba F 6198, Ibrahim Juma Mohamed na kujaribu kunyang’anya siraha aina  ya SMG na katika kurupushani hiyo walimpiga risasi ya begani. 

Amesema askari huyo ameendelea na matibabu katika hospitali ya mnazi mmoja. “ Majambazi walifanikiwa kumpora bunduki aina ya SMG na kasha kumpiga risasi na kumjeruhi begani. Tupo katika msako mkubwa hivi sasa” , amesema kamishana huyo wa polisi Zanzibar. Hata hivyo, alisema wakati mjombo akisonga mbele kujaribu kumsaidia mwenzake, alifyatua risasi lakini ikakwamba katika chemba na majambazi hao kufanikiwa kumpiga risasi sehemu ya ubavu na kutorika. 

Amesema askari huyo wa FFU alifariki majira ya saa 7:00 usiku katika hospitali ya mnazi mmoja na kuzikwa jana huko bambi mkoa wa kaskazini unguja. Watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo na wengine wanaendelea kusakwa.

“Tayari tumepeleka kikosi cha askari maalum kutoka mkoa wa mjini magharibi na mkoa wakusini unguja, ili kuhakikisha usalama unahimarishwa katika maeneo ya ukanda wa utalii”, alieleza kamishana hamdani.

0 Responses to “ASKARI FFU ZANZIBAR AUAWA KWA KUPIGWA RISASI”

Post a Comment

More to Read