Tuesday, March 4, 2014

PACHA MMOJA KATI YA WANNE AFARIKI DUNIA


Mapacha   wa nne waliozaliwa mkesha wa mwaka mpya  (January Mosi mwaka huu) katika hospitali ya Wilaya ya momba na Mwanamke Aida Nakawala(25)  mmoja kati yao amefariki dunia leo baada ya kuugua ugonjwa wa kifua.


MTOTO  mmoja kati ya mapacha wanne waliozaliwa January Mosi mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Momba, amepoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa wa kifua

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkala, amesema motto huyo amefariki  jana majira ya saa kumi na moja za jioni.

Amesema, mtoto huyo ni miongoni mwa mapacha wanne waliozaliwa na mwanamke  Aida Nakawala (25) mkazi wa Chiwanda Wilayani Momba mkoani Mbeya na kwamba chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa kifua.

Aidha, amesema mwili wa marehemu mtoto huyo umezikwa leo katika Kijiji cha Chiwanda na kwamba afya za  watoto wengine watatu waliobakia  zinaonekana si nzuri kwa mujibu wa daktari wa kituo cha afya  kilichopo eneo hilo.

Hata hivyo, amesema  uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana  kuwapeleka mjini watoto watatu waliobakia  kwa  ajili ya matibabu zaidi kwenye hospitali ya wazazi ya meta.

Watoto hao walizaliwa usiku wa kuamkia mwaka mpya January Mosi na mwanamke Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba  katika hospitali ya serikali ya
Momba wakiwa  salama.

0 Responses to “PACHA MMOJA KATI YA WANNE AFARIKI DUNIA”

Post a Comment

More to Read