Friday, March 14, 2014

SITTA: MIMI SIKU ZOTE HUWA MWENYE BAHATI.


mwenyekiti teule wa bunge maalum la katiba samwel sitta ambaye pia ni waziri wa ushirikiano  wa Afrika Mashariki.


Binadamu tunapitia hatua mbalimbali zenye vikwazo furaha na kero hadi kufikia hatua Fulani katika maisha kila mtu ana historia ya maisha yake  kuna walioishi maisha ya taabu na baadaye  kufanikiwa na kuna walioishi maisha ya kifahari tangu  walipoanza  kuwa na akili ya kujua jema na baya  lakini wakiishia na maisha dhahili.

Mmoja wa watu hao ni mwenyekiti teule wa bunge maalum la katiba samwel sitta ambaye pia ni waziri wa ushirikiano  wa Afrika Mashariki.

Mwaka 1961  sitta akiwa na umri wa miaka 19 alishinda shindano la kuandika insha  kwa ligha ya kiingereza kuelezea Tanganyika ikiwa huru ina matumaini gani kwa vijana na akapata zawadi ya kwenda marekani  ambako alikaa kwa muda wa miezi mine.

Mimi siku zote ni mwenye bahati amesema wakati akiongea na mwananchi akizugumzia  shindano hilo sitta amesema mwaka  1961 nilikuwa kijana mdogo sana wakati huo nilikuwa kidato cha nne shule ya sekondari ya wavulana  Tabora.

Shindano hilo la kuandika insha  liliandaliwa na gazeti moja la newyork  marekani na zawadi yake ilikuwa ni kwenda kukaa marekani miezi minne baada ya kushidna nilikwend ahuko na kubahatika  kusoma kule secondary za nchi hiyo.

Amesema alifurahia fursa hiyo kwa sababu ilimwezesha kukutana na Rais wa Marekani wakati huo John Kennedy.

Nilifika katika jengo la ikulu ya marekani  na kutokana na bahati hiyo hata binti yangu wa kwanza nilimuita jina la mtoto wa kike wa kennedy ambaye anaitwa caroline.

Binti huyo wa wa kennedy ni balozi wa marekani nchini japan alisema.

Sitta amesema anakumbuka wakati aanashuka kwenye ndege alidondokewa na barafu tukio hilo hajalisahau.

0 Responses to “SITTA: MIMI SIKU ZOTE HUWA MWENYE BAHATI.”

Post a Comment

More to Read