Friday, March 14, 2014
SERIKALI YAINGILIA KATI ADA VYUO VIKUU.
Do you like this story?
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa |
Serikali imekunjua makucha yake katika
kudhibiti ada zinazotozwa katika vyombo vya utoaji elimu chini.
Akizindua mfumo huo jijini Dar es Salaam, Dk. Kawambwa amesema Serikali imeanzisha mfumo huo unaotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu katika vyuo vyote, kwa lengo la kudhibiti ada kulingana na fani zinazotolewa.
“Sasa natarajia nitapata usingizi wa kueleweka maana kelele za viwango vya ada zilikuwa ni kubwa, kila chuo kilikuwa na ada yake. Niliulizwa vigezo vinavyotumika kupanga sikuwa na jibu, lakini sasa nitakuwa na majibu tena yanayoeleweka,” alisema.
Suala la viwango vya ada katika shule na vyuo binafsi liliwahi kuzungumziwa kwa kina siku za nyuma, huku Rais Jakaya Kikwete na Waziri Kawambwa wakinukuliwa kwa nyakati tofauti kutaka taasisi za elimu kupunguza viwango vya elimu. Aprili 2013 akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyokuwa vya Serikali (Tamongsco) uliofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete alisema: “Elimu ni huduma muhimu na haki kwa mtoto. Siyo vyema kugeuzwa kuwa biashara ya kuleta faida kubwa.’
’
Aliongeza kuwa Serikali ilikuwa katika mchakato wa kutathmini ada zinazotozwa vyuoni na sekondari ili kupendekeza viwango halisi vinavyopaswa kutozwa.
Kwa sasa udadisi wa gazeti hili umebaini kuwa wanafunzi walioanza masomo katika mwaka wa fedha 2013/2014 wanatozwa ada kuanzia Sh360,000 kwa mwaka hadi Sh9,900,000.
Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, mfumo huu ambao baadaye utaendelea hadi shule za sekondari na msingi, umepatikana kupitia kikosi kazi cha wataalamu ambacho pamoja na majukumu mengine kilipewa kazi ya kutathmini gharama.
Dk. Kawambwa alisema moja ya faida ya utaratibu huo mpya ni kudhibiti taasisi zinazotoza ada kubwa kwa sababu za binafsi ikiwamo biashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YAINGILIA KATI ADA VYUO VIKUU.”
Post a Comment