Wednesday, April 16, 2014
AZAM WAJIBU MASHAMBULIZI KUHUSU KUNUNUA UBINGWA.
Do you like this story?
Zikiwa zimepita takribani siku nne
tangu Azam FC ilipoandika historia ya bingwa wa mpya wa ligi kuu ya Vodacom
huku tetesi zikizidi kuzunguka mitaani kwamba klabu hiyo ya jijini Dar es
Salaam imekuwa ikihonga sana wachezaji wa timu nyingine pamoja na marefa ili
kujihakikishia ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa kabisa.
Leo hii kupitia ukurasa wa wa Facebook,
Azam FC wameposti taarifa ya kujibu mashambulizi dhidi yao kwamba wamenunua
ubingwa kwa kuandika:
“Maneno
yanayozungumzwa ni porojo Baada ya Azam Fc kupata mafanikio ya kuwa bingwa wa
ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata nafasi ya pili mara Mbili katika
Ligi Kuu ya Tanzania bara haikuwai kusemwa imenunua leo iweje imekuwa Bingwa
isemwe imenunua.
John Bocco ameweka
Historia Baada ya Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho ya Ligi Daraja la
kwanza na Kuipandisha Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara, na leo Hii
Tumeshuhudia John Bocco ameweka Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa
Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi
kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014 na kucheza Bila kupoteza hata mechi
Moja.
Hatuto puuzia mechi
ya mwisho Dhidi ya JKT Ruvu Tutacheza kama mechi nyingine Tulivyocheza
Tunahitaji kuweka Historia ya Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu Huu JKT
Ruvu wajiandae kwa Kichapo wakati Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu Huu
Baadhi ya Maneno
ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha
katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AZAM WAJIBU MASHAMBULIZI KUHUSU KUNUNUA UBINGWA.”
Post a Comment