Tuesday, April 1, 2014
BARRICK WAIMARISHA MAHUSIANO NA JAMII HUKO KAHAMA.
Do you like this story?
MAHUSINO
baina ya Kampuni ya African Barrick Gold Mines Ltd inayomiliki mgodi wa dhahabu
wa Bulyanhulu wilayani Kahama uliokuwa umetetereka na kuzua migogoro na jamii
inayozunguka mgodi yanazidi kuimarika kutokana ma mabadiliko ya uongozi wa
Idara ya Mahusiano ya Jamii.
Hayo
yalibainishwa juzi na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Ramadhani Madese,
alipozungumza na waandishi wa habari ofisini mwake na kudai hali ya sasa
hivi ni shwari kutokana na idara ya mahusiano ya mgodi huo kukaa na wananchi
kwa maelewano jinsi ya kumaliza kero zinazojitokeza.
Alieleza
awali idara ya mahusino ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana na maamuzi yake
kuyafanya kibabe, hali iliyozua migogoro ya mara kwa mara na wananchi ambao
wakati mwingine walikuwa wakiziba barabara kuzuia magari na shughuli za mgodi
zisifanyike.
Hata
hivyo, alisema kwa kipindi hiki idara hiyo ya mahusiano inayoongozwa na Meneja
wake, Abdallah Msika, aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga
imekuwa na mahusiano mazuri kiasi cha kumudu kufanya marekebisho makubwa kwa
wananchi wanaozunguka mgodi huo, hali iliyofanya kuimarisha usalama eneo la
mgodi.
Na Ali Lityawi-Kahama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BARRICK WAIMARISHA MAHUSIANO NA JAMII HUKO KAHAMA.”
Post a Comment