Tuesday, April 1, 2014

WAKUTUBI WALIA NA UHABA WA VITABU.










Watoa huduma na utunzaji wa kumbukumbu Maktaba ya Mkoa wa Mbeya.



WATOA huduma za Maktaba Mkoa wa Mbeya, wamesema licha ya serikali ya kuwa na mkakati wa   kusogeza huduma kwa wananchi hadi ngazi ya Tarafa lakini bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitabu vya nukuu.

Hayo yamesemwa  leo jijini Mbeya  na Mkutubi msaidizi wa maktaba ya Mkoa wa Mbeya, Florence Mwambeso wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya huduma za Maktaba Tanzania.

Amesema  Bodi ya makataba inatarajia kujenga majengo pamoja na kusambaza vitabu mpaka ngazi ya Tarafa hatua mbayo italeta mafanikio makubwa kwa Taifa kuwa na wasomi wengi lakini tatizo lililopo ni uhaba wa vitabu vya nukuu kwa uapande wa wanafunzi wa sekondari na vyuo  vya elimu ya juu.

Amesema, lengo la bodi ni kuhakikisha inatekeleza mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa hivyo kitendo cha kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi kiende sambamba na usambazaji wa vitabu kwenye maktaba hizo.

Amesema, changamaoto kubwa wanayoipata  watoa huduma kwenye maktaba hizo ni ukosefu wa vitabu hasa vya nukuu hivyo wateja huzalimika kutumia muda mwingi kwa kuwasubili wengine wamalize ndipo nao wachukue na kuanza kusoma.

Aidha, amesema mbali na tatizo hilo pia maktaba za mikoani  zipo nyuma kiutandawazi tofauti na za binafsi ambazo hutoa  fursa kwa msomaji kutumia mitandao endapo kitabu husika hakitakuwepo.

Hata hivyo, Mwambeso ameiomba serikali kushughulikia suala hilo ili kuongeza idadi ya watu kwenda kujisomea ikiwa na kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa

0 Responses to “WAKUTUBI WALIA NA UHABA WA VITABU.”

Post a Comment

More to Read