Tuesday, April 1, 2014

MALI ASILI NA UTALII YAFANIKISHA KUPUNGUZA UJANGILI KWA ASILIMIIA 58, WAKAMATA MENO YA TEMBO,NA MIZOGA YA TEMBO 39.




WIZARA ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana  na wadau wengine hapa nchini wamefanikiwa kuendesha doria ambayo iliweza kufanikisha kupungua kwa kasi ya ujangili hapa nchini kwa asilimia 58 tofauti na mwaka jana ambapo ujangili ulikuwepo kwa kiwango cha juu sana 

Aidha doria hiyo ya Mandays pia iliweza kufanikisha kukamatwa kwa mali gahafi ambazo zilikuwa zkitumika na majangili hayo ambayo  yamekuwa yakisababisha madhara makubwa sana kwa taifa la tanzania Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mkurugenzi wa idara ya wanyama pori  taifa  Paulo Sarakikya alidai kuwa  oparesheni hiyo ilianza rasmi toka januarya hadi kufikia mwezi machi mwaka huu na takwimu zinaonesha mafanikio makubwa sana kwani doria hiyo pia iliweza kuhusisha ujangili wa ndani na hata ule wa nje ya hifadhi.

Aliendelea kwa kusema kuwa katika kipindi husika jumla ya mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani na nje ya hifadhi za taifa na mapori ya akibanchini huku meno mazima yakiwa ni 171 na vipande 22 vya meno ya tembo ghafi , vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62  pamoja na nyama pori zenye jumla ya kilo 1,111 ambazo nazo zilikuwa ni kwa ajili ya vitoweo vya majagili hayo.

Sarakikya alidai kuwa mbali na kukamata vitu hivyo pia waliweza kukamata vitu vingine kama vile
Bunduki ya rashasha  moja, Rifle 3, shotgun 2, gobori 5 na jumla ya risasi 7 za aina mbalimbali  pamoja na malighafi kama vile  magari 5  ngombe 2663 misumeno 1 na mbao 745

0 Responses to “MALI ASILI NA UTALII YAFANIKISHA KUPUNGUZA UJANGILI KWA ASILIMIIA 58, WAKAMATA MENO YA TEMBO,NA MIZOGA YA TEMBO 39.”

Post a Comment

More to Read