Tuesday, April 1, 2014
MTOTO WA MIAKA 2 AMUOKOA MAMAKE.
Do you like this story?
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili
nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake
kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.
Wahudumu wa afya katika kituo cha
kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa afya
walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''
Wahudumu hao walifanikiwa kwenda
nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza
mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.
Walimfanyia upasuaji wa dharura
baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu
nyingine kutoka katika kizazi chake.
Sasa mtoto huyo Riley Ward
amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo
ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo.
Mamake , Dana Henry, alimtaja
mwanawe kama shujaa wake mdogo.
Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema
kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga
simu.
Pia alisema kuwa ameweza
kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na
mumewe hawahisi vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTOTO WA MIAKA 2 AMUOKOA MAMAKE.”
Post a Comment