Tuesday, April 1, 2014
DPP awarudisha kizimbani ‘Wafungwa wa Magufuli’
Do you like this story?
Wafungwa wawili raia China waliokuwa wakitumikia
kifungo cha miaka 20 kwa kosa la uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa
Bahari ya Tanzania (Exclussive Economic Zone- EEZ), maarufu kama wafungwa wa
Samaki wa Magufuli, wamefunguliwa upya mashtaka.
Wafungwa hao, Hsu Chin Tai, ambaye alikuwa
nahodha wa meli ya Tawaliq iliyokamatwa ikifanya uvuvi huo haramu, na aliyekuwa
wakala wa meli hiyo, Zhao Hanquing, waliachiwa huru na Mahakama ya Rufani
Ijumaa iliyopita.
Hata hivyo, jana walipandishwa tena kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa upya mashtaka ya awali
yaliyowapeleka gerezani.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwarudisha
tena kizimbani na kuwasomea upya mashtaka hayo baada ya Mahakama ya Rufani
kutengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyowatia hatiani awali, kutokana na kasoro za
kisheria katika kuwashtaki.
Katika hukumu yake, Mahakama ya Rufani
ilisema mwenendo wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu ulikuwa batili kutokana kosa
walilolifanya kutokusikiliza hoja za upande wa utetezi kuwa washtakiwa
walifunguliwa mashtaka hayo bila kibali cha DPP.
Hata hivyo, Mahakama ya Rufani ilitoa nafasi
nyingine kwa DPP kuwafungulia upya mashtaka hayo kwa kufuata utaratibu kama
angependa kuendelea na mashtaka dhidi yao.
Hatua ya DPP kuwarudisha kizimbani tena
Wachina hao na kuwasomea mashtaka hayo inamaanisha kuwa kesi hiyo inaanza upya
tangu hatua ya kwanza, kama vile walikuwa hawajawahi kushtakiwa kwa makosa
hayo.
Katika kesi hiyo mpya namba 13 ya mwaka 2014
inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Warialwande Lema, washtakiwa hao walisomewa
mashtaka mawili yanayowahusu wote kwa pamoja wakati mshtakiwa wa pili Hanquing
akikabiliwa na shtaka moja zaidi.
Washtakiwa hao jana walisomewa mashtaka hayo
na Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila akisaidiana na mawakili wengine wa
Serikali Tumaini Kweka, Hamidu Mwanga na Rose Chilongzi.
Katika shitala la kwanza, washtakiwa hao
wanadaiwa kufanya shuguli za uvuvi katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kibali, kinyume cha kifungu cha 18 (1) cha
Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi Katika Kina Kirefu cha Bahari.
Wakili Mwangamila alidai kuwa Januari 10,
2009 na Machi 8, 2009, washtakiwa hao kwa pamoja walifanya shughuli za uvuvi
katika eneo la Tanzania bila kuwa na leseni.
Katika shtaka la pili wanadaiwa kufanya
uchafuzi wa maji na mazingira ya bahari eneo la Tanzania kinyume cha Kanuni (1)
(2) na kanuni ya 70 ya Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi katika kina kirefu cha bahari
mwaka 2009.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DPP awarudisha kizimbani ‘Wafungwa wa Magufuli’”
Post a Comment