Tuesday, April 1, 2014
KWELI SERIKALI ITADHIBITI ADA KUBWA VYUONI?.
Do you like this story?
Kwa muda mrefu wananchi wa kada mbalimbali
wamekuwa wakilalamika kuhusu karo kubwa zinatozwa shuleni na katika vyuo vya
elimu ya juu.
Kuna shule hapa nchini ambazo ada yake kwa
mwaka inazidi kiwango kinachotozwa katika baadhi ya vyuo vikuu.
Hata hivyo, tatizo linatajwa kuwa kubwa zaidi
kwenye vyuo vikuu. Kwa mfumo ulivyo nchini wanafunzi wanapoomba nafasi vyuoni,
wanaweza kupangiwa chuo chohote.
Hali hii imekuwa ikiwaathiri wanafunzi
wanaotoka katika familia masikini, kwa sababu wanajikuta wamepangiwa chuo
kinachotoza karo kwa kiwango kikubwa.
Vyuo ni tofauti na shule kwa sababu mzazi
ndiye anayeamua wapi ampeleke mwanawe kulingana na uwezo wa fedha alionao.
Inawezekana hili linalotokea katika taasisi
za elimu ya juu ndilo lililoisukuma Serikali kuanzisha kile ilichokiita kama
mfumo mpya wa upangaji ada kwa vyuo vikuu.
Akizindua mfumo huo hivi karibuni, Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema utasaidia kudhibiti
viwango vya ada vinavyotozwa kwa wanafunzi.
Alisema Serikali imeanzisha mfumo huo
utakaoanza kutumika mwaka huu katika vyuo vyote, kwa lengo la kudhibiti ada
kulingana na fani zinazotolewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KWELI SERIKALI ITADHIBITI ADA KUBWA VYUONI?.”
Post a Comment