Tuesday, April 1, 2014
UKAWA WAANZA MAPAMBANO NJE YA BUNGE.
Do you like this story?
Dar /Dodoma/Mwanza. Ni dhahiri kwamba mjadala wa msomi wa Sheria, Profesa
Issa Shivji umewavuruga wanasiasa waumini wa serikali mbili ambao baadhi yao
jana walimshukia wakidai kuwa “mzee huyu ni ndumila kuwili na kigeugeu.”
Shivji juzi alitoa mjadala kuhusu muundo wa
Muungano na kuishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopendekeza serikali
tatu, kuwa ilipotosha maoni ya wananchi. Alipotakiwa kuzungumzia madai dhidi
yake, Profesa Shivji alisema: “Nyie ni waandishi wa habari someni, angalieni
wapi mimi nilisema Serikali tatu, wanaosema ninatumiwa na CCM hayo ni maoni yao
siwakatazi kuzungumza wanachofikiria.”
Jana Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
katika kampeni yake nje ya Bunge la Katiba, ulimtaka Profesa Shivji kuwaomba radhi
wananchi kwa kile wanachodai kwamba amekuwa kigeugeu kwenye maandishi na
matamshi yake kuhusu muundo wa Muungano.
Katika mkutano wake wa kuelimisha wananchi
kuhusu Katiba Mpya mjini Mwanza uliojaa polisi kila kona, Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema wanamshangaa Profesa Shivji kwa mawazo yake
yasiyoeleweka kuhusu muundo wa Muungano.
“Kwa kweli tunaamini watu ambao ni wasomi
kama Profesa Shivji wanaweza kuwasaidia wananchi kupata katiba nzuri, lakini
anachokifanya sasa ni siasa, jambo ambalo siyo jema,” alisema Dk. Slaa na
kuongeza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UKAWA WAANZA MAPAMBANO NJE YA BUNGE.”
Post a Comment