Saturday, April 26, 2014
JUKWAA LA KATIBA WATANGAZA KUSULUHISHA MGOGORO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Do you like this story?
Waandishi wa Habari wakifuatilia. |
Jukwaa
la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano miongoni
mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi
zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum
la katiba Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es
Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba juu ya tathimini
walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano
hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki akiwemo
mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye
atakuwa mkuu wa jopo hilo la usuluhisho na ndugu Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.
Aidha
jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni
uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje
lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo
jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia
sheria.
Kibamba
amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia
wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku
akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais siku ya
tarehe 26 mwezi huu yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura
mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba
mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje
ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano
kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili
kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JUKWAA LA KATIBA WATANGAZA KUSULUHISHA MGOGORO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.”
Post a Comment