Wednesday, April 2, 2014

JUSSA ADAI SITTA ANAWAPENDELEA WAJUMBE.




Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ismail Jussa Ladhu anaendelea kulia na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kuwa anawaburuza.


Jussa alitoa kauli hiyo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma alipozungumza 

Alilalamikia uongozi kuwa umepanga kuliburuza Bunge hilo.
Anacholalamika mjumbe huyo ni namna ambavyo wamekuwa wakitafuta nafasi za kuchangia lakini Mwenyekiti anatoa nafasi kwa wachache na kuwaacha wajumbe ambao wanatoka upande wa upinzani.

Jussa alisema wakati wanapitisha Kanuni, wajumbe wengi ambao ni wabunge na wajumbe kutoka Baraza la Wawakilishi hawakupewa nafasi ya kuchangia kutokana na kuwa walikuwa ni wajumbe wa CUF.

“Nikikupa orodha utaona mwenyewe kwamba katika upande wa CUF, alipewa nafasi Rukia Kassim pekee licha ya kuwa tuliomba zaidi ya 10,” alisema Jussa.

 Hata hivyo, Sitta alikanusha tuhuma hizo na kusema shida inayowakumba baadhi ya wajumbe ni kutiliana mashaka pasipokuwa na ushahidi.

“Hapa  watu wanatiliana mashaka bila ya kujua kinachoendelea mbele, hatuwezi kupanga orodha kama anavyosema mjumbe katika masuala ya Kanuni, wakitaka wasubiri kwenye Rasimu, hivi sasa kila  kitu kinazuka palepale,” alisema Sitta.
“Wajumbe wa CCM walipewa zaidi ya nafasi tano, huu ni uonevu,” alisema Jussa.

Alimtuhumu Sitta kuwa anapendelea na kugawa nafasi hiyo kwa wajumbe wa CCM pekee jambo linalotoa tafsiri kuwa, wamelenga kupata Katiba ya upande mmoja.

Alilalamikia kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge kutogawa orodha ya wachangiaji wakati kanuni zinasema hivyo, jambo analosema linamfanya Mwenyekiti kupoteza sifa.

0 Responses to “JUSSA ADAI SITTA ANAWAPENDELEA WAJUMBE.”

Post a Comment

More to Read