Wednesday, April 2, 2014
MSANII KULALA NDANI YA TUMBO LA DUBU.
Do you like this story?
Abraham Poincheval akipanda ndani ya Dubu wake kabla ya kuonyesha atakavyojifungia ndani |
Abraham Poincheval akichunguza ndani ya Dubu wake katika makavazi ya wanyama waliowindwa na kuhifadhiwa. |
Msanii mmoja nchini Ufaransa anajiandaa
kulala ndani ya tumbo la Dubu wake aliyewindwa na kuhifadhiwa katika makavazi
ya wanyamapori mjini Paris.
Uamuzi wake huu umetajwa kama kuchagua kati
ya maisha ya binadamu na wanyama.
Msanii huyo mfaransa anaanza maonyesho yake
ya kiusanii ambayo yametajwa kuwa ya kipekee na ambayo yatashuhudia akilala
ndani ya mnyama huyo kwa siku 13.
Abraham Poincheval aliyezaliwa mwaka 1972 kwa
mara ya kwanza alifanya maonyesho hayo yanayojulikana kama -kuishi ndani ya
ngozi ya Dubu- katika kituo cha maeonyeso ya usanii mjini Digne mwaka jana.
Sasa anajiandaa kurejelea onyesho hilo katika
makavazi mjini Paris ambako atasalia ndani ya tumbo la Dubu huyo ambaye ni
mnyama halisi isipokuwa tu amekaushwa na kuhifadhiwa katika makavazi hiyo. Poincheval
aliwahi kuishi ndani ya shimo chini ya maktaba mjini Marseilles Oktoba mwaka
2012.
Inaarifiwa mwanaume huyo ni mjuzi wa
maonyesho ya usanii yenye kutumia mbinu hatari.
Poincheval atakula, kulala na hata kwenda
haja akiwa ndani ya tumbo la Dubu huyo, huku akinaswa na kamera mbili.
Duru zinasema kuwa kilichompa Poincheval motisha
ya kuishi ndani ya mzoga wa mnyama huyo, ni mizoga ya wanyamapori aliyokuwa
anakutana nayo mara kwa mara nchini Ufaransa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSANII KULALA NDANI YA TUMBO LA DUBU.”
Post a Comment