Friday, April 25, 2014
SIKU 67 ZA MIPASHO, MATUSI BUNGENI.
Do you like this story?
Bunge
Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila
kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
Badala
yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta “Mzee wa Kasi na Viwango”
linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya
Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya
Muungano unaopendekezwa.
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa
Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.
Kutokana
na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni
mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa
Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa
kudhibiti hali hiyo.
Mwanzoni
mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba
ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka
kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
“Mwenendo
wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote za kuonyesha kungetokea matatizo ndani
yake kutokana na mipasho ambayo ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha
ambazo siyo za staha wakati wa kutengeneza kanuni,” amesema Oluoch na kuongeza:
“Kwanza
matumizi ya lugha zisizo na staha, mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja
kwa kupeana mipasho bila kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni,” alisema
Olouch.
Hata
hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha Bunge hilo kwa umakini mkubwa na
kwamba kila anaposikia lugha chafu amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru
kufuta kauli au kuomba radhi kwa matamshi. “Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo
mojawapo ya mambo ambayo huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango
inapotolewa na wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili,
kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu,” alisema Suluhu.
Alikiri
kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi
na kwamba masuala yao hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya
kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.
Sehemu
ya Tano ya Kanuni za Bunge Maalumu inatoa mwongozo wa mambo yanayokatazwa na
yale yanayopaswa kufuatwa wakati wa mjadala.
Kanuni
ya 46 imeorodhesha mambo yasiyoruhusiwa ambayo ni pamoja na kusema uongo, kutoa
taarifa zisizokuwa za kweli, kuzungumza jambo lolote ambalo halipo kwenye
mjadala na kutumia majina ya marais na waasisi wa Taifa kwa dhihaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIKU 67 ZA MIPASHO, MATUSI BUNGENI.”
Post a Comment