Monday, April 28, 2014

SIMBA YANYAKUWA WACHEZAJI WAWILI KUTOKA MBEYA CITY FC,AKIWEMO KASEKE.


Kikosi cha Simba


Deus Kaseke


Wekundu wa Msimbazi Simba Spots  Club ya jijini Dar es Salaam yadaiwa kuchukua wachezaji wawili machachari toka club ya Mbeya  City Fc ya jijini Mbeya.

Wachezaji wanaodaiwa kuchukuliwa na Wekundu hao ni pamoja na Saad Kipanga na Deus Kaseke ambao wanatajwa kuwa tegemezi kubwa kwa Timu hiyo ya Mbeya City .
Kwa mujibu Chanzo Chetu cha habari  kimedai  kuwa tayari mazungumzo baina ya wachezaji  hao wa Mbeya City na uongozi wa Simba yamekwisha fanyika ambapo kwa sasa yapo  hatua nzuri.

Chanzo hicho kimedai kuwa mazungumzo ya wachezaji hao yalianza mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa Tanzania Prisons na Rhino Rangers ya mjini Tabora  uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini hapa.

Amesema mazungumzo hayo yalikuwa kati ya wachezaji hao pamoja na baadhi ya viongozi na kocha mkuu wa Simba .
Pia Chanzo hakikuwa wazi kuweka bayana juu ya mkataba huo kwani muda gani pamoja na mshahara watakayolipwa wachezaji hao licha ya kudai kuwa ni mshahara mnono tofauti na walichokuwa wakilipwa awali na Mbeya City.

Kufuatia hali hiyo Fahari News blog imepata fursa ya kuzungumza na uongozi wa mbeya city juu ya kuwepo kwa tetesi hizo.

Afisa habari wa Timu hiyo ya Mbeya City Ndugu Frady Jackson  amedai kuwa taarifa zinazozungumzwa juu ya kuuzwa kwa wachezaji hao si zakweli kwani wao bado wanatambua kuwa wachezaji hao ni mali yao hasa kutokana na mikataba yao ambayo imeweka wazi.
Amesema yeye  kwa upande wake kama msemaji wa Timu hiyo bado haja pata taarifa zozote juu ya  kuuzwa kwa wachezaji hao licha ya kuendelea kuzisikia  kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Amesema klabu hiyo haijakataza kwa mchezaji yoyote kusajiliwa na Timu nyingine inayoshiriki Ligi kuu lakini zipo taratibu za kufuatwa ili mchezaji awe huru kuchezea timu nyingine au kusajiliwa kabisa nasi vinginevyo kama inavyo dhaniwa na baadhi ya wadau.

Amesema hata kama mchezaji atasaini mkataba na club hiyo ya Simba na nyinginezo  lakini bado wao kama viongozi hawalitambui hilo kwani bado hayajafanyika mazungumzo yoyote kati ya Uongozi wa Simba na Mbeya City.

“Nikweli Ndugu Mwandishi hatukatai  kwa mchezaji yoyote kusajiliwa na Timu nyingine lakini zipo taratibu zake za kusajili mchezaji hawezi tu akaingia makubaliano naTimu nyingine pasipo uongozi wa wetu kufahamu,”Alisema afisa Habari huyo.

Amebainisha kuwa kama kutafanyika kwa mazungumzo baina ya Club  hizo mbili ambazo ni Mbeya City na Simba natumaini kuwa akitoaribika  kitu kwani kila mtu ana uhuru na anaangalia maslahi .

Club hiyo ya Mbeya kwa mara ya kwanza imeshiriki Ligi kuu Tanzania Bara 2013/14  na kuleta upinzani mkubwa katika ligi hiyo ambapo mpaka ligi inakwisha Club hiyo ilishika nafasi ya Tatu tofauti na Simba ambayo ilishika nafasi ya Nne.

0 Responses to “SIMBA YANYAKUWA WACHEZAJI WAWILI KUTOKA MBEYA CITY FC,AKIWEMO KASEKE.”

Post a Comment

More to Read