Monday, April 28, 2014
WANAFUNZI 111 WAPATA MIMBA MKOANI LINDI.
Do you like this story?
Jumla ya wanafunzi 111 wamepata mimba kwa
kipindi cha mwaka 2012/13 katika shule za msingi na sekondari mkoani
Lindi na 1405 kati ya 8399 waliochaguliwa kujiunga elimu ya sekondari mwaka huu
mkaoni Lindi hawajafika kwenye shule hizo kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo utoro,
Hayo yamebainishwa na afisa elimu
mkoa Silas Semaluku alipokuwa anazungumza na wadau wa elimu kwenye
mkutano wa wadau wa Elimu mkoani Lindi.
Semaluku alisema mkoa una kabiliwa na
changamoto kubwa za watoto kupata mimba kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo tamaa kwa watoto wakike kuwa na vitu vya thamani ambazo zimeanza
kufanyiwa kazi , na idara ya elimu pamoja na wazazi,
Alisema wilaya Lindi inaongoza kwa kuwa
na watoto wengi waliopata ujauzito ambao 48 ikifuatia wilaya Kilwa 23,
Nachingwea 18, Ruangwa 14, Liwale 6 na manispaa ya Lindi 2.
Semaluku alisema kuwa mkoa ulipangiwa
wanafunzi 8,399 kati yao wasichana 4,078 na wavulana 4,321 lakini waliofika
shuleni hadi sasa ni 6,994 pia wanafunzi 1,405 hawajafika shule hadi sasa
kati yao wavulana 720 na wasichana 685.
Alifanunua kuwa wanafunzi halmashauri
ya wilaya Lindi kuna wanafunzi 327 wahajafiki shule hadi sasa, Liwale
wanafunzi 230, Kilwa 200 Ruangwa 351 wilaya ya Nachingwea 226 huku Manispaa ya
Lindi ikiwa na wanafunzi 69.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI 111 WAPATA MIMBA MKOANI LINDI.”
Post a Comment