Wednesday, May 21, 2014
17 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI BORNO,NIGERIA
Do you like this story?
Watu
17 wameuawa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya kijiji kimoja Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria.
Mji
wa Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu na mji wa Chibok ambako
wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu
la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Hili
ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria wakati nchi hiyo
ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana miambili waliotekwa
nyara na Boko Haram.
Juhudi
hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel, Marekani
na Uingereza.
Pia
limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika jimbo
la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi
za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi
wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos, lilisababishwa
na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali kuwa wapiganaji hao
wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “17 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI BORNO,NIGERIA”
Post a Comment