Wednesday, May 21, 2014
TAPELI SUGU AKAMATWA NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA.
Do you like this story?
Akiwa Chini ya Ulinzi Mkali. |
Kijana
Mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mwinyi na Kujitambulisha anatokea
VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi la polisi kwa Ushirikiano na Madreva wa
Wabunge hapa Dodoma kwa tabia yake Mbaya ya Kutapeli watu.
Kijana
huyo amekuwa akijihusisha na Matukio Mbalimbali ya Utapeli hapa Dodoma kwa
nyakati tofauti na kwanji tofauti na kwa watu tofauti.Utapeli wake amekua
akiufanya kwenye Uuzaji wa Viwanja akijidai yeye ni Dalali wa Viwanja,Pia
amekamatwa akiwa na Fungo "FAKE" za Gari ambazo amekuwa akitumia
kutembea nazo na kujidai yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma hivyo anahitaji
Msaada,Kwa nyakati tofauti Madreva wamekuwa wakikutana naye na kuwaomba masaada
na hatimaye Kupewa fedha za Kumuwezesha Kurudi Dsm alikosema ndio anafanya kazi
ya TASAF.
Lakini
hadi jana anakamatwa akiwa kwenye jaribio la Kumtapeli Dreva wa Mh:Makongoro
Mahanga, ameshadanganya Madreva Wengi na bado amekuwa akionekana Dodoma
tofauti na maelezo yake kuwa anahitaji msaada wa Nauli arejee Dsm tangu Bunge
la Katiba Kuanza,Pia ameshukiwa kutapeli watu wengi fedha likiwamo jaribio la
Kuiba pikipiki eneo la Kituo cha Polisi Dodoma.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Rai,Kama
Umetapeliwa hapa Dodoma,tafadhali fika Kituo cha Polisi Dodoma Mjini kwa msaada
zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAPELI SUGU AKAMATWA NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA.”
Post a Comment