Wednesday, May 21, 2014

BAADA YA KIKOMBE CHA BABU SASA NI DHAHABU SAMUNGE.




Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la samunge wilaya ya ngorongoro mkoa wa aursha safari hii siyo kunywa kikoche cha babu mchungaji  ambilikile mwasapile bali kupata dhahabu inayodaiwa  kugundulika katika eneo hilo.

Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi  kumiminika katika kujipatia madini hatyo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za mto katika kijijji cha mgongo kilichopo jirani na kwa babu.

Diwani wa samunge Jackson sandea  alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika  katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu  yanapatikana hapo.

Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka hii inaweza kuwa nai zaidi ya kipindi kile cha babu wa kikombe. Dhahabu  hii inapatikana mtoni tu watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu  hakuna mtu ambaye anachimba alisema sandea. Alisema tofauti na maeneo mengine dhahabu ya samunge ina onekana ni ya watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na serikali na ndiyo sababu wanaingia kwa wingi. Kuna wenginawanapta hata mashambani  lakini mtoni ndipo inapoptikana kwa wingi zaidi alisema.

Ulinzi waimarishwa
Diwani huyo alisema ulinzi umeanz a kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo kunaweza kutoke vurugu kubwa na hata mauaji.

Sisi kama viongozi tumeweka utaratibu mzuri wa kuchumba madini kiusalama  na hata wale ambao wameanza kuuza mashamba yao tunawawekea  utaratibu mzuri alisema.

Maofisa madini kutua samunge
Kamishna wa madini kamanda wa kaskazini alex magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu katika eeno la samung maofis wake wanajidandaa kwenda kijijini hapo.

Alisema taarifa za kitaalamu kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo samunge itatolewa baada ya maofis hao kufika katika eneo hilo na kufanya utafiti.

Ahadi ya babu
Kugundulika dhahabu katika eneo hilo kunahusishwa na ahadi ya mchungaji  msapila kuwa mamilioni   yawatu watafika tena samung e bada ya kupungua ikilinganishwa na miezi ya mwanzao baada ya kuanza kutoa tiba ya kikoche cha dawa iliyodaiwa kutibu mgonjwa sugu.

Licha ya wengi kuitilia shaka kauli yake hiyo aliendelea kusisistiza na akakta miti na kujenga kituo kikubwa cha kutolea huduma ya kikombe.

0 Responses to “BAADA YA KIKOMBE CHA BABU SASA NI DHAHABU SAMUNGE.”

Post a Comment

More to Read