Wednesday, May 21, 2014

DENGUE YADAIWA KUGEUKA MARADI UBUNGO




Hatua ya upulizaji wa dawa ya mbu katika mabasi imezua mgawanyiko  miongoni mwa wadai baada ya kudaiwa kugeuza mradi wa wachache kutokana na kiwango kikubwa cha fedha kinachotozwa.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa mko wa dare s salaam said meck sadiki kwa ajili ya kudhibiti ueneaji wa mbu  wanaobeba vimelea vya ugonjwa wa homa ya dengue kutoka jijini humo kwenda mkoani.

Tuhuma hizo zimetolewa na baadhi ya wamiliki wa mabasi yanaodai hawajashirikishwa katika utekelezaji wa mpango huo hasa kuhusu gharama y ash 65,000 zinazotozwa kwa kila basi.

Sakata hilo lilianza jana alfajiri kwa baadhi ya mabasi  yaliyokuwa yameanza safari zao bila kupulizwa dawa kurudishwa ndani ya stendi ili kutekelza agizo hilo.

Abiria walikuwa wanapatwa na usumbufu  mkubwa baada ya mabasi yao kuzuiwa kuondoka kwa sababu hayakuwa ymepulizwa  dawa na kubandikwa stika za mamlaka ya usafirishani majini na nchi kavu (Sumatra) pia kulikuwa na madi kuwa baadhi ya mabasi yalilipa fedha sh 65,000 na kununua stika hizo kasha kuendelea na safari zao bila kupulizwa dawa tuhuma ambazo meneja wa lesini wa Sumatra , leo ngowi amesema hana taarifa nazo.


Amesema hata Taboa(chama cha wamiliki wa mabasi) ambao wanadiwa wameshirikishwa siyo kweli na kama hili limefanyika ni kwa viongozi wachache wa umoja huo.

Meneja ngowi wa Sumatra amesema baada ya majadiliano baina yake na utawala wa stendi hiyo na wadau wakiwamo taboa wameamua kutoa siku zaidi  hadi ijumaa iwe mwisho na ambaye atakuwa hajapuliza dawa hataruhusiwa kusafirisha abiria.

Alisema sh 65,000 siyo kaisi kikubwa na kuwa katika kipindi hicho wenye mabasi watakuwa wanategemea mamilioni ya fedha hivyo ni vyema wakati agizo hilo ili kusiaidia kuzuia sambamba kwa homa hiyo mkoani.

0 Responses to “DENGUE YADAIWA KUGEUKA MARADI UBUNGO”

Post a Comment

More to Read