Wednesday, May 21, 2014

NUNDU: VIGOGO SERIKALINI WAPEWA NYUMBA NA WAGENI




Waziri wa zamani wa uchukuzi omar nundu jana aliikalia kooni serikali kwa kuwakumbatia wageni na kuibua madai kuwa baadhi ya vigogo wa seriali walipewa nyumba wakati wa kubinafsisha viwanda  nchini.

Nundu ambaye ni mbunge wa tanga mjini (CCM) alitoa kauli hiyo jana jioni alipokuwa akichangia  bajeti ya waziri wa viwanda  na biashara, DK Abdallah kigoda kwa mwaka 2014/15 tax hliday (kipindi maalumu cha kusamehewa kodi) ziondolewe maana siyo tunasema maneno tu  umefika wakati sasa maneno yakae kando vitendo vifanye kazi watu wamechukua viwanda kwa ajili ya kuvidhoofisha  tu alisema.

Tanga kule vimejaa chungu nzima(viwanda) na tunapoongelea maji tu tunayajua mliyoyafanya . vipomlivyopewa kutoka viwanda vile ondoeni mawazo hayo msitupeleke mpaka  tukasema mambo haya humu ndani amesema nundu na kuongeza:

Nundu amesema uchumi duniani kote unategemea viwanda na kwamba pamoja na wizara kueleza mambo mengi ukweli ni kwamba hayatoshi na kuna mengi ya kufanya.

Utajiri wa magadi
Awali akiwasilisha bajeti yake waziri wa viwanda na biashara DK Abdallah kigoda lisem uzlaishaji wa magadi  soda utaanza kuliingizia taifa doda 320 milioni nza marekani(sh 520 bilioni) kwa mwaka kuanzia mwaka 2016/17.

Alisema mradi huo unaoendeshwa na shirika la maendeleo ya taifa (NDC) unatarajia kuzalisha tani milioni moja za madini hayo na bidhaa nyingine  za chumvi kwa mwaka. Alisema tafiti  kuhusu wingi na ubora wa rasilimali ya magadi soda zilikamilika mwaka 2013/14 na kiasi cha tani bilioni 4,68 za magadi ambazo huongezeka  kwa mita za uajzo milioni 1.86 ziligunduliwa.

Dk kigoda alisema kiasi hicho kiligunduliwa ktika bonge la engaruka na jitihada za kumtafuta mtaalamu mshauri zimeanza.


0 Responses to “NUNDU: VIGOGO SERIKALINI WAPEWA NYUMBA NA WAGENI”

Post a Comment

More to Read