Wednesday, May 21, 2014
MAJAMBAZI YAPORA FEDHA KAWE CLUB.
Do you like this story?
Mtu mmoja
ambaye hakutaka kujulikana jina lake amekumbwa na mkasa wa kuvunjiwa na kuibiwa
pesa kiasi kisichopungua shilingi za kitanzania milioni 10 alipokuwa katika
mgahawa wa Kawe Club jijini Dar es Salaam
Akielezea
tukio hilo, shuhuda ambaye pia hakutaka kutajwa jina lake anasema ilikuwa
majira ya saa kumi na nusu wakati majambazi wasiopungua watano
walipovunja kioo upande wa kushoto mbele cha gari aina ya Toyota Hilux
yenye usajili T163CUL na kuchukua hela kiasi cha shilingi milioni 10.
“Walikuja
na pikipiki wakati mi naosha gari hiyo, nikiwa upande wa pili (yaani wa dereva)
naosha tairi ya mbele, nikasikia mshindo wa kuvunjwa kioo, nikaona watu wawili
kwenye pikipiki mmoja ameshika bunduki wakichukua pesa kwenye gari na kisha
wakaondoka mbio” alieleza kijana huyo.
Kijana
huyo anasema alipiga kelele za wezi, walinzi wakiwa wanashangaa hawajui la
kufanya. Kwa mujibu wa kijana huyo, kelele zake zikasaidia kwani watu
wanaofanya shughuli zao eneo la baharini karibu na Kawe Club walisikia na
kuanza kuwakimbiza watu hao.
Walipofika mbele kidogo wakiwa wanawakaribia, ndio jambazi mmoja akapiga risasi hewani ndipo watu wote wakalala chini kuhofia usalama wao.
Kijana mwingine aliyekuwa anapita njia ya kuelekea Kawe Beach anasema aliposikia kelele ya risasi kisha akaona pikipiki gari aina ya RAV4 zikifuatana kwa mwendo mkali sana.

Imedaiwa tukio zima lilichukua si zaidi ya dakika tatu
mpaka watu hao kutokomea. Hata hiyvo meneja wa Kawe Club alifanikiwa kuita
polisi ambao walifika muda si mrefu kufuatilia tukio hilo.
Mmiliki wa gari hilo anasema alikuwa ametoka benki ya CRDB Mlimani City kuchukua pesa hizo na ndipo alipoamua kwenda kula samaki Kawe Club kabla ya kukumbwa na mkasa huo.
“Nikiwa ndani nikasikia alam ya gari inalia, lakini pia nilisikia makelele ya watu walidai mwizi mwizi, ndo kutoka nikakuta wameshatokomea. Wamefanikiwa kuchukua hela pekee lakini wameacha silaa yangu iliyokuwa katika droo ya gari, nafikiri hawakujua kama ipo lasivyo na yenyewe ingekwenda” alieleza mtu huyo

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAJAMBAZI YAPORA FEDHA KAWE CLUB.”
Post a Comment