Sunday, May 4, 2014

BOMU LALIPUKA TENA MOMBASA NA KUUA WATU.





Watu watatu wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Mombasa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari ambao hupendwa kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.

Mlipuko mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.

Kamishna mkuu wa polisi Mombasa, Nelson Marwa, amesema watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu waliotekeleza shambulizi hilo walitoroka kwa Pikipiki.

Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.

Aidha nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu wapatao 67.

Al Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na yale ya Umoja wa Afrika AMISOM.

CHANZO: BBC

0 Responses to “ BOMU LALIPUKA TENA MOMBASA NA KUUA WATU.”

Post a Comment

More to Read