Sunday, May 4, 2014
WIMBO MPYA WA WANAHABARI WAZINDULIWA ARUSHA SAMBAMBA NA ALBAMU YA MRISHO MPOTO.
Do you like this story?
Jaji mstaafu Mark Bomani jana (leo )amezindua rasmi video ya
wimbo
wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja
na
albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto
ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru
wa vyombo vya habari duniani.
Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti yangu kamera
yangu leo ndio kaburi langu mie.Huo ndio wimbo wa
kundi la Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa ukiwaburudisha wanahabari
katika uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto Band,unaoelezea mambo mbalimbali
wanayokumbana nayo wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni sana misa
Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano
tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake
Akiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo huo wa
wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale
alivyofatwa na wanahabari na kumuomba awatungie wimbo ambao
unawahusu wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili.
Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi yake kuwa
watu wasanii wengi wamekuwa wakizindua albamu kwa
kuweka viingilio vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi
ameamua kuzindua albamu hii katika siku hii ya waandishi wa
habari kwa kuwa wamemtoa mbali na anakitu cha kuwapa zaidi ya
kuwapa zawadi hii ya kuzindua albamu yake mbele yao.
Alibainisha kuwa mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa
waandishi wamempa hadhi
ya kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa waandishi wa
habari ndani ya albamu yake ili kila mtanzania na
mshabiki wake ambaye atanunua albamu yake aukute wimbo ndani
ya albamu yake.
"Hii
albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na wimbo wa
nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli
najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu
na ata jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani
kuwa hii kwangu itakuwa ni historia katika maisha yake"alisema
mpoto
Katika wakati wimbo huu ukiendelea wanahabari walionekana wakitoa
machozi kwa kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani
msanii huu ameuimba kiualisiazaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WIMBO MPYA WA WANAHABARI WAZINDULIWA ARUSHA SAMBAMBA NA ALBAMU YA MRISHO MPOTO.”
Post a Comment