Sunday, May 4, 2014

TAIFA STARS YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MALAWI SOKOINE MBEYA, YATOKA 0-0





Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr Noman Sigara (wa tano kutoka kulia)Ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika Mpambano huo wakiwa na viongozi wa timu zote wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa wa Malawi.

Timu ya Malawi

Timu ya Taifa Stars

Ujumbe kutoka kwa mashabiki.


TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimisha suluhu pacha ya bila kugungana na timu ya Taifa ya Mawali katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wengi kiasi jijini Mbeya tofauti na inapocheza Mbeya City fc, Taifa stars iliyosheheni wachezaji wazoefu imeshindwa kupata matokeo ya ushindi.

Stars walipata nafasi za kufunga, lakini safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na John Raphael Bocco `Adebayor` ilishindwa kuzibadili kuwa mabao.

Malawi nao walionekana kuwa na mipango mizuri na kulifikia lango la Stars mara nyingi, lakini uimara wa kipa Deogratius Munish `Dida` ulisaidia.

Almanusura John Bocco aandike bao katika dakika ya 20 kipindi cha pili kwa shuti kali, lakini mpira uligonga mwamba.
Dakika ya 33 kipindi cha pili Malawi walifanya shambulizi kali, lakini Dida aliokoa.

Kocha mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameanza kazi yake kwa suluhu, lakini imekuwa kipimo kizuri kwake kujua makali ya kikosi chake ambacho kiliweka kambi tangu aprili 27 mwaka huu,  mjini Tukuyu kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni harakati za kujiweka sawa kabla ya kuanza kusaka tiketi ya kushirki kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.

Hii ni mechi ya pili ya kirafiki kwa Stars ya maboresho ambapo mechi nyingine walicheza  Aprili 26 mwaka huu dhidi ya Burundi na kuchapwa mabao 3-0 na akina Didier Kavumbagu, Amisi Tambwe na Yusuf Ndikumana wa Burundi.

Huo ulikuwa mchezo maalum wa  kuadhimisha miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibara ambapo timu ya taifa ya Burundi iliizidi kwa kila kitu Taifa stars iliyosheheni wachezaji wengi kutoka kikosi cha maboresho.

0 Responses to “TAIFA STARS YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MALAWI SOKOINE MBEYA, YATOKA 0-0”

Post a Comment

More to Read