Tuesday, May 13, 2014
DAWA YA MENO KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME.
Do you like this story?
Kemikali
zinazopatikana katika baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa
ya kusugua meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua
zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.
Kwa
mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo
wa mbegu za uzazi za wanaume kuzalisha mwanamke.
Wanasayansi
hao wanasema kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya
uzazi kwa wanaume katika nchi za magharibi.
Kemikali
zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu
za kiume kuweza kuzalisha.
Takriban
mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la
kuzalisha na tatizo la utasa ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.
Uchunguzi
huu ulifanywa na watafiti kutoka Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi
kemikali 100 kila siku huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo
ziliathiri uwezo wa Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.
Utafiti
huu uliandikwa katika jarida la afya la EMBO na watafiti wanasema nyingi ya
kemikali hizo hatari zinapatikana katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale
hatari ya jua.
Kemikali
nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa
ya kusugua meno.
Uchunguzi
wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta
mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika
kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za
mwanamke.
Mabadiliko
haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha.
Watafiti
hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo
.
Kemikali
hizi hujulikana kama kemikali zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya
kemikali zinzzoathiri homoni za mwili wa mwanamume.
Mwaka
jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na
pumu.
BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DAWA YA MENO KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME.”
Post a Comment